STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, leo ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Mohammed Chande Othman kuwa Mjumbe na kushiriki vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.
Kiapo hicho kimeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri na maafisa wengine wa serikali
Mara baada ya kula kiapo hicho, Rais Wa Zanzibar amehudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Kikwete.
Jioni ya leo, Rais Kikwete anatarajiwa kuelekea Perth, Australia kuhudhuria Kikao cha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kinachofanyika kuanzia tarehe 28-30 mwezi huu.
Rajab Mkasaba, Dar-es-Salaam
No comments:
Post a Comment