Kocha Jan Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambao wataanza kwenye mechi ya leo dhidi ya Morocco. Mechi hiyo inaanza saa 1.30 usiku kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania ni saa 4.30 usiku na itachezwa Grand Stadium hapa Marrakech. Poulsen atatumia mfumo wa 4-4-1-1 huku akimweka Mbwana Samata kuwa mshambuliaji wa mwisho na nyuma yake akicheza Abdi Kassim.
Katika kikosi cha kwanza amewaanzisha wachezaji wote wa kulipwa wanaocheza nje ya Tanzania ambao anao hapa. Amewataka wachezaji kuwa focussed na mchezo, kujituma na kila mmoja kutekeleza wajibu wake uwanjani ili ushindi uweze kupatikana. Baada ya kutoa game plan yake, Poulsen aliwaonesha wachezaji CD ya mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Morocco ambapo tulifungwa bao 1-0.
Kupitia CD hiyo aliwaeleza wachezaji upungufu uliojitokeza na pia wachezaji hatari wa Morocco wanaotakiwa kuangaliwa kutokana na uzuri wao wanapokuwa uwanjani. Amewakumbusha mabeki kuwa mshambuliaji Chamakh Marouane (Arsenal, Uingereza) kuwa ni mzuri kwa mipira ya vichwa, hivyo kutomuacha kuruka peke yake katika mipira hiyo.
Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Mohamed Rajab, Henry Joseph (Captain), Mbwana Samata, Abdi Kassim na Dan Mrwanda. Subs: Shabani Dihile, Nassoro Cholo, John Bocco, Ramadhan Chombo, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Jabir Aziz
No comments:
Post a Comment