Sunday, October 9, 2011

MABALOZI NA WAWAKILISHI WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA WAELEZA KURIDHISHWA NA JITIHADA ZA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

MAELEZO Butiama, Mara
Na Ismail Ngayonga 
MABALOZI na wawakililishi wa mashirika ya kimataifa hapa nchini wameleeza kuridhishwa kwao na jitihada za Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na kuimarisha dhana ya utawala bora nchini.
Akisoma risala ya mabalozi hao leo wakati waliotembela kaburi na makazi la Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi wa Mabalozi hao, Balozi Juma Mpango alisema mafanikio hayo yametokana na misingi imara uliojengwa, Mwalimu Nyerere.
Balozi Mpango alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika zinaheshimika kutokana na jitihada zake za kuwaunganisha pamoja wananchi wake na kuendelea kuimarisha umoja, amani, utulivu na mshikamano.
Aliongeza kuwa Tanzania pia imeendelea kusifika na kuheshimika katika jumuiya ya kimataifa kutokana na utawala wake kutoegemea mfumo wa itikadi za udini na ukabila, jambo ambalo kwa kiasi limekuwa likisababisha hali ya vita na machafuko katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika.
“Tanzania Bara inaadhimisha miaka 50 ya uhuru, jambo kubwa la kijuvunia ni kwamba hakuna kikundi cha watu wanaoweza kushika hatamu za madaraka pekee na lugha ya Kiswahili nayo imekuwa ni kiungo cha watu” Alisema B alozi Mpango huku akimwagia sifa Mwasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa mujibu wa Balozi huyo alisema Bara la Afrika na dunia kwa ujumla itaendelea kudhamini mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kwani alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mataifa yote ya Bara hilo yanapata uhuru wake kutoka kwa wakoloni.
Naye Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania Bara inaadhimisdha miaka 50 ya uhuru wake huku ikijivunia kuwa miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika lisilopigana vita vya wenyewe kwa wenyewe, misingi ambayo imeachwa na Baba wa Taifa mwalimu Nyerere.
“Tazama katika mataifa mengine ya Bara la Afrika leo hii nchi hizo zimeingia katika vita na akina mama na watoto wamekuwa wahanga wakubwa, lakini kwetu sisi Tanzania ni tofauti leo hii tunaishi kwa upendo bila ya ubaguzi wa dini wala kabila” alisema Waziri Membe.
Waziri Membe alisema kutokana na Mabalozi waliopo nchini kuguswa na historia ya Mwalimu Nyerere katika harakati zake za ukombozi wa Bara la Afrika, hivyo waliamua kutembelea kijiji chake cha Butiama pamoja na kuangalia kaburi alilozikwa kiongozi huyo, aliyekuwa mwanaharakati wa ukombozi wa Bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment