Monday, November 21, 2011

DR. SHEIN AMTEUA MTORO ALMASI KUWA KATIBU WA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA, ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Mtoro Almasi Ali kuwa Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdul Hamid Yahya Mzee imesema kuwa Rais amaefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 22 cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Zanzibar, No. 2 ya Mwaka 2011

Kabla ya Uteuzi huo Mtoro Almas aliwahi kufanya kazi akiwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Soda Zanzibar, Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Zanzibar na kuwa Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha TUNGUU Zanzibar.

Mtoro Almas ana Stashahada ya Juu ya Utawala aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro na Shahada ya Uzamili aliyoipata Uingereza.

Uteuzi huo umeanza Novemba 20, Mwaka huu

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
21/11/2011

No comments:

Post a Comment