Wednesday, November 23, 2011

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAY YAAGWA NA KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA TAYARI KWA CHALLENGE

Waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Abdilah Jihad Hassan akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Agrey Moris huko kikwajuni mjini zanzibar katika sherehe za kuwaaga wachezaji wa timu hiyo wanaokwenda kweye michuano ya Tusker Cecafa Challenge Cup 2011
Waziri wa Habari Utamaduni utalii na michezo akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar katika hafla ndogo ya kuwaaga iliyofanyika kikwajuni mjini zanzibar kushoto ni naibu waziri wa habari utamaduni utalii na michezo Bihindi Hamad Khamis na kulia ni Rais wa chama cha soka cha zanzibar Ali Fereji tamimu
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar heroes wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya habari pamoja na viongozi wa chama cha soka cha Zanzibar

Na Hamad Hija Maelezo Zanzibar

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Jihad Abdilah Hassan amsema kuwa timu ya taifa ya Zanzibar ni timu yenye uwezo mkubwa na anaamini kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika michuano ya kombe la challenge itakayoanza wiki hii huko jijini Darsalaam

Waziri Jihad ameyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Wizara ya habari ulioko Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati akiiaga na kuikabidhi bendera timu ya Taifa Zanzibar, Zanzibar Heroes inayokwenda kushiriki michuano ya challenge.

Waziri huyo wa habari amefafanuwa zaidi na kusema kuwa lengo la kushiriki mashindano kwa timu hiyo, ni kuleta ushindi na kwa kuwa timu imeandaliwa vizuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma, inasababu kubwa ya kufanya vizuri.

Waziri amesema, hivi sasa timu ya Zanzibar Heroes inatisha kutokana na maandalizi makubwa yaliyofanywa na timu hiyo,ikiwemo kuweka kambi ya wiki mbili Nchini Misri hatua ambayo ni sababu ya msingi kwa timu hiyo kuipeperusha vyema b endera ambayo wamekabidhiwa.

AidhaWaziri Jihad amesema kuwa mashindano ni mashindano hivyo timu iwemakini katika kucheza mpira na ifuate sheria kumi na saba za mchezo ndicho kitu pekee ambacho kitawasaidia wakati wa michezo na wakati mashindano yanapoendelea nchini humo.

Aidha Waziri amesema kuwa mashindano ni sawa na vita hivyo timu ya Taifa ya Zanzibar inatakiwa ipigane kufa na kupona ili iweze kufanya vizuri katika michuano hiyo ya challengeambayo yanafanyika jijini Darsalamm ikiwa inazishirikisha timu za ukanda huu wa Afika Mashiriki ambapo timu ya Somalia Uganda Kenya Tanzania ni miongoni mwa timu zinazotegemewa kushiriki katika mashindano hayo

Na kwa upande wa kocha wa timu hiyo ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar heroes) Hemed Suleiman Moroko amesema kuwa, kwa mara ya pili wanategemea kulileta kombe hilo hapa Zanzibar kwa vile timu hiyo imepata maandalizi ya kutosha

Amesema kuwa kwa mara ya kwanza timu ya Taifa ya Zanzibar ilileta kombe mwaka 1995 kutoka Nchini Uganda na mwaka huu wa 2011 timu hiyo na kukusudia kuleta tena kombe hilo kutoka Tanzania bara.

Naye Kapteni wa timu hiyo ya Taifa ya Zanzibar Agrey Moris, amewaahidi wananchi wa zanzibar kwamba wataipeperusha vyema bendera ya Zanzibar,kutokana na kuwa wamejipanga vizuri katika michuano hiyo ya kombe la challenge linalotegewa kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii


Wakati huo benki ya watu wa Zanzibar PBZ imetowa jumla ya shilingi millioni mbili ikiwa ni mchango wao kwenye timu hiyo ya Taifa fedha hizo zimekabidhiwa leo katika hafla hiyo ya kuagwa kwa timu ya Taifa na Meneja Masoko wa benki hiyo ya Zanzibar Juma Amuor ame

No comments:

Post a Comment