Tuesday, November 22, 2011

TAIFA CHANGA KAMA TANZANIA LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA VIJANA AMBAO HAWAWEZI KUJITUMA NA KUJIAJIRI: HAJI USSI

Na Nafisa  Madai       Maelezo Zanzibar

Mkuu wa idara ya utawala na uwenezi katika chama cha mapinduzi mhe Haji Ussi Gavu amesema taifa changa kama Tanzania linakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokua na vijana ambao wanaoweza kujituma na kujiari wenyewe.

Amesema taifa linakabiliwa na tatizo hilo linaweza kuzorota katika uwendeshaji wa shughuli zake za kila siku kwa kupoteza nguvu ngazi na rasilimali kazi ya vijana ambao wengi hivi wamekua wakijishulisha na kadhia za vigenge.

Gavu ambae pia ni naibu waziri wa miundombinu na mawasiliano ameyasema hayo alipokua akifunga mkutano mkuu wa baraza la vijana  katika wilaya ya Muheza mkaoni Tanga.

Aidha alisema taifa bila ya kuwepo kwa amani na utulivu linaweza kukosa amani hivyo aliwaasa vijana hao walinde amani na utulivu uliopo kwa sasa kwani uzoefu unaonesha vijana ndio vyanzo vya migogoro katika mataifa mbali mbali.

Hata hivyo alisema imani yake kubwa utulivu uliokuwepo unaletwa na CCM lakini kuna baadhi ya vyama kwa makusudi wanachochoe vijana katika vyuo  kufanya vurugu jambo ambalo limekua likitishia amani katika nchi hii.

“Matendo yanayoyafanywa na baadhi ya vyama vya siasa ni vya ajabu sana leo hii wanachochea vijana tena wanafunzi katika vyuo vikuu  hii dalili tosha  ya uharibifu wa amani katika chii yetu.””alisema Gavu.

Aidha aliwataka vijana hao waelekeze nguvu zao katika kilimo kama ilivyo azma ya serikali ya kutaka kuinua kilimo na kusema KILIMO KWANZA mbapo alisema iwapo watafanya hivyo changamoto  ya umaskini itawaondoka.

Aidha alisema  ili kujenga jeshi kubwa la kilimo lazima vijana wajitolee katika kilimo ili rasilimali iweze kubaki nchini na isichukulie

No comments:

Post a Comment