Tuesday, November 8, 2011

POLISI ARUSHA WAMSHIKILIA DKT SLAA,TUNDU LISU, MBOWE NAYE ASAKWA NA POLISI

NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA
Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia wafuasi wa chadema 20 akiwemo katibu wa chama cha chadema Dkt Wilboard Slaa pamoja na mbunge wa Singida Bw Tundu Lissu,huku mwenyekiti wa chama hicho Bw Freeman Mbowe akiwa ametoroka na kwa kosa la kukiuka masharti ya jeshi la polisi cha kufanya mkutano wa hadhara kwa masaa matano na badala yake wakakesha katika viwanja vya NMC mjini hapa kwa ajili ya shinikizo dhidi ya mbunge wa arusha mjini kinyume cha sheria

Akiongea na vyombo vya habari kaimu kamanda wa jeshi hilo kwa mkoa wa Arusha Bw Akili Mpwapwa alieza kuwa watu hao ambao ni watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka hilo kwa kuwa wamekiuka kwa makusudi masharti ya kibali chao

Kamanda mpwapwa ameendelea kwa kusema kuwa mnamo tarehe saba chama cha demokrasia na maendeleo kilipewa kibali maalumu cha kuweza kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya NMC lakini badala yake chama hicho kwa kuongozwa na viongozi wa ngazi za kitaifa walipuuzia suala hilo na kufanya mkesha huku wakiwa wanaendelea kutoa lugha za kejeli kwa serikali.

Aliendelea kudai kuwa viongozi hao kwa kushirikiana na wananchi waliamua kufanya mkesha maalumu juu ya kushinikizwan kuwekwa rumande kwa mbunge wa jimbo la arusha mjini ambapo wafuasi hao walikesha huku kibali cha mkutano huo kikiwa tayari kimeshakiwisha 

“Hawa chadema walivunja utaratibu huo tena kwa kujua kabisa kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kwa kuwa kibali kilikuwa kinajieleza wazi juu ya kutokusanyika baada ya masaa matano kuisha, kutokashifu dini au chama kingine,pia kutokuwa na maandamano ya magari au pikipiki lakini walikiuka agizo hilo alisema Akili.

Kamanda huyo aliongeza kuwa mara baada ya watu hao kukaa kwa zaidi ya masaa mengi huku mji ukiwa na tafrani kubwa sana ya kutokea kwa vita polisi waliamua kuchukua maamuzi kwa maslahi ya wananchi wa Mkoa wa arusha na hivyo kuweza kuwatanya watu hao.

Pia alisema kuwa viongozi hao wa chadema waliendelea na lugha za kejeli na kuonesha ukaidi dhidi ya sheria za nchi wakati nao polisi wakiendelea kuwasihi wasitishe mkuatano huo ambao ulidumu mpaka alfajiri lakini bado viongozi hao walikiuka amri hiyo.

Aliongeza kuwa mnamo majira ya alfarjiri polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuweza kuwatanya watu jambo ambalo nalo lilifanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu sana na wafuasi hao wakaweza kukimbia na kutawanyika katika eneo hilo la NMC.

‘tulipoingia uwanjani hapo na kutumia zaidi nguvu watu walikimbia sana lakini bado sisi tulilenga kuwakamata baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa chama hicho ambapo Dkt slaa alikutwa akiwa amejificha chini huku Mbunge wa singida Tundu Lisu naye akijisalimisha kwa jeshi la polisi, mwenyekiti wa chama hicho akitokomea kusikojulikana”aliongeza kamanda Mpwapwa.

No comments:

Post a Comment