Saturday, September 17, 2011

WATU 47 WAUAWA SYRIA


Kwa mujibu wa ripoti za wanaharakati wa upinzani, hadi watu 47 waliuawa na vikosi vya usalama vya Syria hapo jana, baada ya waandamanaji kumiminika barabarani katika sehemu mbali mbali nchini humo.

Kama raia 21 waliuawa katika wilaya ya Idlib karibu na mpaka wa Syria na Uturuki.
Kwa mujibu wa wanaharakati hao wa upinzani, vikosi hivyo vilikuwa vikifyatua risasi ovyo na wenyeji hawakuweza kuwasaidia majeruhi.
Wengine 6 waliuawa Hama na vifo vingine vilitokea mji mkuu Damascus, Homs na Deir Ripoti hizo haziwezi kuthibitishwa na vyombo huru vya habari kwani serikali ya Syria imewapiga marufuku waandishi wa habari wa kigeni.

No comments:

Post a Comment